Open top menu
Jumatatu, 14 Oktoba 2013


USHINDI wa Ivory Coast dhidi ya Senegal umekuwa hatua muhimu ya kuelekea katika Fainali za Kombe la Dunia.
             
Mabao 3 yaliyofungwa na washambuliaji Didier Drogba, Gervinho na Salomon Kalou yametosha kuiongezea matumaini Ivory Coast ya kushiriki fanali za kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil.

Goli la kufutia machozi upande wa Senegal lilifungwa kimiani na mshambuliaji wa NewCastle Papiss Demba Cisse.

Mechi ya mkondo wa pili itachezwa mwezi ujao nchini Morocco kwa sababu Senegal inatumikia adhabu ya kutochezea kwenye uwanja wa nyumbani.

Katika mchezo mwingine, penalti ya dakika za mwisho iliyopewa Burkinafaso katika mazingira ya kutatanisha iliiwezesha timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Algeria.

Hadi dakika ya 85 matokeo yalikuwa magoli 2-2 kabla ya Burkinafaso kupata penalti iliyowawezesha kuondoka na ushindi mdogo.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments