Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool kutoka Tanzania,
Patrick Nyangusi (kushoto) akiwa na mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika
Kusini kabla ya kuanza mchezo wa fainali uliofanyika jijini Blantyre nchini
Malawi mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool kutoka Tanzania,
Patrick Nyangusi akicheza dhidi ya mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika
Kusini (hayupo pichani) wakati wa mchezo wa fainali uliofanyika Blantyre Malawi
mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Taifa ya Safari
Pool ya nchini Tanzania wakiwa wamembeba mchezaji,Patrick Nyangusi mara baada
ya kutwaa ubingwa wa Afrika wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) kwa kumfunga
Vishen Jagdev wa Afrika Kusini 6-4,katika mchezo uliofanyika Blantyre Malawi
mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Safari Pool kutoka
Tanzania wakishandilia na mchezaji Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa
ubingwa wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) Afrika uliofanyika Blantyre Malawi
mwishoni mwa wiki.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya
Tanzania wakiwa na medali zao za Fedha mara baada ya kutunukiwa kwa kupata
nafasi ya tatu katika mashindano ya Pool Afrika yaliyofanyika jijini Blantyre
Malawi mwishoni mwa wiki
Mgeni rasmi, Mjumbe wa Baraza la Michezo Nchini
Malawi, Sharaf Pinto(wa pili kushoto) akiwa na mabingwa wa Singles(mchezaji
mmoja mmoja).Kutoka kulia ni mshindi wa tatu kutoka Zambia, Moses Mofya,mshindi
wa pili kutoka Afrika Kusini, Vishen Jagdev na Bingwa gwa Afrika kutoka
Tanzania, Patrick Nyangusi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kuwakabidhi medali zao Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Mabingwa wa Afrika
wa mchezo wa pool wakiwa katika picha nya pamoja. Kutoka kushoto ni
Bingwa wa Afrika kutoka Tnzania, Patrick Nyangusi,mshindi wa pili kutoka Afrika
Kusini, Vishen Jagdev na mshindi wa tatu kutoka Zambia, Moses Mofya mara baada
ya kukabidhiwa zawadi zao jijini Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa Afrika wa Safari Pool kutoka Tanzania,
Patrick Nyangusi akiwa katika picha ya pamoja na warembo wa Blantyre Malawi
mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya medali ya zahabu mwishoni mwa wiki.
0 comments