MABINGWA mara nne wa Afrika, TP Mazembe imefanikiwa
kutinga kwenye hatua ya fainali bila ya kuwa na nyota wake watatu wa Zambia,
baada ya kuinyuka CS Sfaxien ya Tunisia bao 1-0 mchezo uliochezwa jijini
Lubumbashi jana.
Mazembe wamefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya
kushinda kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya kushinda mabao 2-1 katika mchezo wa
kwanza uliochezwa jijini Tunis wiki mbili zilizopita.
Shukrani kwa bao la Kiungo wa DR Congo, Tresor Mputu
na kuwahakikishia timu yake kucheza mchezo wa nfaiunali ambao utachezwa mwezi
ujao.
Katika mchezo huo TP Mazembe waliwakosa wachezaji
wake, Rainford Kalaba, Nathan Sinkala na Stoppila Sunzu ambao wamezuiliwa nchini
kwao baada ya kugoma kuichezea timu yao ya Taifa ya Chipolopolo dhidi ya Brazil
uliochezwa nchini China wiki iliyopita.
Wachezaji hao ambao waligoma kusafiri na timu hiyo kwa
madai kuwa wanaumwa lakini serikali ya Zambia waliwanyang’anya hati za
kusafiria za wachezaji hao hivyo wakashindwa kusafiri kwenda DR Congo kuitumikia
klabu hiyo.
0 comments