MCHEZAJI wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya
Ghana, Kevin-Prince Boateng atakosa mechi ya mkondo wa kwanza ya kujitafutia
nafasi kucheza Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Misri, kutokana na jeraha la
goti.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alipata
jeraha hilo wakati wa mechi ya klabu yake ya Schalke ya Ujerumani kwenye mechi
za Ligi ya Bundesliga.
Na baada ya kufanyiwa ukaguzi na madaktari,
imegunduliwa kuwa Boateng lazima afanyiwe upasuaji kwenye goti lake la kushoto.
Kocha wa timu ya Black Stars, Kwesi Appiah, ameamua
kutafuta mchezaji mwingine kuchukua nafasi ya Boateng.
Mechi za mkondo wa pili za kufuzu kwa kombe la dunia
litakalochezwa nchini Brazil mwaka ujao, zitachezwa mjini Cairo, Misri tarehe
19 Novemba.
Hata hivyo, Ghana wameomba michuano hiyo kuhamishiwa
kwingineko kwa sababu za usalama kufuatia hali ilivyo nchini Misri.
0 comments