SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) limetoa
majina ya wachezaji 23 watakaowania tuzo za mwanasoka Bora wa Dunia kwa mwaka
2013 ‘FIFA Ballon d’Or’.
Wachezaji hao 23 waliotangazwa watachujwa mwezi
Desemba mwaka huu na kubaki wachezaji watatu ambao wataingia kwenye hatua ya
mwisho ya fainali itakayofanyika Januari 13, 2014 jijini Zurich, Uswisi.
Hicho cha kutoa tuzo hiyo pia kutachaguliwa kikosi
bora cha mwaka, kocha bora, mchezaji bora wa kike, beki bora, golikipa bora,
kiungo na mshambuliaji bora wa dunia.
Majina ya wachezaji hao na nchi zao kwenye mabano ni
Gareth Bale (Wales), Edinson Cavani (Uruguay), Radamel Falcao (Colombia), Eden
Hazard (Ubelgiji), Zlatan Ibrahimović (Sweden), Andres Iniesta (Hispania),
Philipp Lahm (Ujerumani), Robert Lewandowski (Poland), Lionel Messi
(Argentina), Thomas Muller (Ujerumani), Manuel Neuer (Ujrumani), Neymar
(Brazil) na Mesut Ozil (Ujerumani).
Wengine ni Andrea Pirlo (Italia), Franck Ribéry (Ufaransa),
Arjen Robben (Uholanzi), Cristiano Ronaldo (Ureno), Bastian Schweinsteiger (Ujerumani),
Luis Suarez (Uruguay), Thiago Silva (Brazil), Yaya Toure (Ivory Coast), Robin
Van Persie (Netherlands) na Xavi (Hispania).
Kwa upande makocha waliotajwa katika orodha ya
kuwania tuzo ya kocha bora wa dunia nchi zao na timu wanazofundisha kwenye
mabano ni Carlo Ancelotti (Italia/Paris Saint-Germain FC/Real Madrid CF),
Rafael Benítez (Hispania/Chelsea FC/SSC Napoli), Antonio Conte (Italia/Juventus)
na Vicente Del Bosque (Hispania/Timu ya Taifa ya Hispania).
Wengine ni Sir Alex Ferguson (Scotland/Kocha wa
zamani wa Manchester United), Jupp Heynckes (Germany/Kocha wa zamani wa FC
Bayern München), Jurgen Klopp (Germany/Borussia Dortmund), Jose Mourinho (Ureno/Real
Madrid CF/Chelsea FC), Luiz Felipe Scolari (Brazil/Timu ya Taifa ya Brazil),
Arsene Wenger (Ufaransa/Arsenal FC).
0 comments