Open top menu
Jumanne, 22 Oktoba 2013


MABAO matatu ya kusawazisha ya Simba katika mchezo wa watani wa jadi, juzi yamezidi kuitesa Yanga baada ya jana badala ya kuanza mazoezi kujiandaa na mchezo wa kesho walikaa kujadili sababu za kutoka sare katika mchezo huo.

Yanga katika mchezo huo, walitawala mchezo kwa dakika 45 za kwanza na kuwasaidia kupata ushindi wa mabao 3-0 yaliyofungwa na Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza aliyefunga mawili kabla ya Simba kusawazisha katika kipindi cha pili.

Simba ambao waliingia vyumbani wakiwa tayari wamelala kwa mabao hayo matatu, lakini walirudi kwa kasi na kufanikiwa kusawazisha mabao yote matatu na kufanya mchezo huo umalizike kwa matokeo ya sare.

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts jana aliwakarisha chini wachezaji wake na kuwataka mmoja baada ya mwingine aeleze sababu ya mchezo huo kumalizika kwa sare wakati wao wakiwa wameshamaliza mchezo huo katika kipindi cha kwanza.

Brandts alimtaka mchezaji mmoja mmoja aeleze kile anachokijua kwanini wameshindwa kushinda katika mchezo huo na ndipo wachezaji hao walipoanza kufunguka.

Lakini baadhi ya wachezaji wakiwemo Jerry Tegete na Didier Kavumbagu waliumtaka kocha wao waache kujadili kwani hakuna sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa sababu ya kutoka sare ni uzembe ya baadhi ya wachezaji wenzao.

Pamoja na maombi hayo ya Tegete na Kavumbagu lakini Brandts aliwataka waendelee kutoa maoni yao na baada ya kumaliza ndipo mazoezi yaliendelea.

Kesho Yanga itavaana na Rhino Rangers mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Simba watakuwa mjini Tanga kupepetana na Coastal Union.

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments