MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji
Simba na Tanzania Prisons kutoka Mbeya iliyochezwa jana (Oktoba 12 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 60,521,000.
Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi
hiyo namba 55 na kushuhudiwa na watazamaji 10,494 waliokata tiketi kwa
viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Kila klabu ilipata mgawo wa sh. 14,191,002.55 wakati
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,232,016.95.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya
uwanja sh. 7,215,763.96, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh.
4,329,458.37, Kamati ya Ligi sh. 4,329,458.37, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 2,164,729.19 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 1,683,678.26.
0 comments