TIMU ya Arsenal jana imeyaaga mashindano ya Capital
One baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Chelsea katika mchezo wa
hatua ya mtoano ya michuano hiyo, uliochezwa kwenye Uwanja wa Emirates jijini
London.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa
vijana wa Jose Mourihno walianza kupata bao la kwanza kupitia kwa beki wake wa
kulia, Mhispania Cesar Azpilicueta akitumia vizuri makosa ya Carl Jenkinson
aliyerudisha mpira mfupi kwa kipa wake, Lukasz Fabianski na kunaswa na mfungaji
na kukwamisha mpira wavuni.
Arsenal walicharuka mara baada yta kuruhusu bao hilo
lakini waishindwa kupenya ngome ya Chelsea na kujikuta wanaenda mapumziko
wakiwa nyuma kwa bao hilo moja.
Wakiwa katika mipango ya kusawazisha bao hilo
Arsenal walijikuta wanafungwa nao la pili kwa shuti kali la Juan Mata ambalo
lilijaa moja kwa moja wavuni na kumuacha kipa asijue nla kufanya.
Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo, Manchester
United waliishushia kipigo cha mbwa mwizi timu ya Norwich City cha mabao 4-0 na
kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Mabao ya Manchester yalifungwa na Javier Hernandez ‘Chicharito’
mawili, Fabio na Phil Jones na kuwafanya timu hiyo kutinga hatia hiyo kwa
ushindi mnono.
West Ham United waliibuka na ushindi wa mabao 2-0
dhidi ya Burnley wafungaji wakiwa Matt Taylor kwa penalti na Jack Collison, nao
Stoke City walivuka hatua hiyo baada ya kuiondosha Birmingham City kwa mikwaju
ya penalti 4-2 baada ya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya 4-4 katika dakika
120.
0 comments