BAADA ya kuichapa timu ya Kagera Sugar kwa mabao 2-1
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika mjini Bukoba mwishoni mwa
wiki, jana kikosi cha Yanga kilirejea jijini Dar es salaam na leo asubuhi
kikitua kisiwani Pemba ambapo kitakua kambini kwa muda wa wiki moja.
Yanga inaweka kambi kisiwani Pemba ikiwa ni mara ya
pili mfululizo katika mchezo wake dhidi ya watani wa jadi Simba SC, ambapo
kambi ya awali iliwafanya vijana wa jangwani kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
yaliyofungwa na Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza 'Diego'.
Msafara wa watu 38 wakiwemo wachezaji wote 29
waliosajiliwa kwa ajili yakuichezea Yanga msimu huu na viongozi 9, watakua
kisiwani Pemba katika maandalizi ya mchezo huo ambao ni muhimu kwa Yanga ili
kujiweka katika mazuri ya kuongoza Ligi Kuu na baadae kuteteta tena ubingwa
wake.
Mara baada ya kuwasili kisiwani Pemba leo asubuhi
kwa ndege tatu za kukodi kikosi kimefanya mazoezi yake ya kwanza katika uwanja
wa Gombani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba SC Oktoba 20,
2013.
Ikiwa ni takribani siku sita kabla ya kupamba na
Simba SC siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam, kikosi
cha Mholanzi kimeamua kuweka tena kambi katika visiwa hivyo tulivu kwa lengo la
kusaka ushindi.
Kocha Mkuu Ernie Brandts amesema anatambua kikosi
chake kinakabiliwa na mchezo mgumu, haswa ikizingatiwa wanapokutana watani wa
jadi mechi huwa inakuwa ngumu sana lakini kwa sasa anakindaa kikosi chake ili
kiweze kuendeleza wimbi la ushindi.
"Pemba ni sehemu nzuri, tulikuwepo huku
mwishoni mwa msimu uliopita kwa ajili ya maandalizi dhdi ya Simba na tuliibuka
na ushindi wa mabao 2-0, uwanja wa mazoezi mzuri na hali ya hewa ni nzuri
vitatutaongeza chachu ya ushindi kufuatia kuwa sehemu tulivu" alisema
Brandts
Wachezaji waliondoka kwenda Pemba ni makipa, Ally
Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida' na Yusuph Abdul, mabeki ni Mbuyu
Twite, Juma Abdul, Issa Ngao, David Luhende, Oscar Joshua, Nadir Haroub
'Cannavaro', Kelvin Yondani 'Cotton', Rajab Zahir na Ibrahim Job.
Viungo ni Athuman Idd 'Chuji', Frank Domayo, Salum
Telela, Bakari Masoud, Haruna Niyonzima, Nizar Khalfani na Hamis Thabit wakati
washambuliaji ni Mrisho Ngassa, Saimon Msuva, Abdallah Mguhi 'Messi', Didier
Kavumbagu, Hamis Kiiza, Jerson Tegete, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Reliants
Lusajo na Shaban Kondo.
0 comments