MCHEZAJI soka wa Nigeria, Nosa Igiebor alijeruhiwa
vibaya wakati timu yao iliposhambuliwa mjini Addis Ababa baada ya mchuano wao
wa mchujo dhidi ya Ethiopia katika kutafuta nafasi ya kushirki kombe la dunia
mwaka ujao nchini Brazil.
Mchezaji huyo ambaye huchezea timu ya Real Betis
alihitaji matibabu ya dharura mkononi mwake baada ya dirisha la basi walimokuwa
kuvunjwa wakati timu hiyo ilipokua inaondoka katika mji mkuu Addis Ababa. Alijeruhiwa
kwa vioo.
Nigeria, ilishinda mabao mawili kwa moja na
wameripoti tukio hilo kwa Fifa.
"Tunatumai kuwa Fifa itachukua hatua za
kinidhamu," alisema Makamu Rais wa Shirikisho la Soka la Nigeria, Mike
Umeh. "Ni jambo la aibu sana kwa tukio kama hili lilitokea baada ya mechi.”
Ben Alaiya, Afisa wa uhusiano mwema wa timu ya taifa
ya Super Eagles alimuunga mkono Umeh katika kulaani tukio hilo.
Alaiya alisema kuwa mashabiki walishambulia basi
iliyokuwa imewabeba wachezaji wa timu ya Nigeria kwa mawe ambayo yalivunja mojawapo
ya dirisha la basi hivyo kulazimisha wachezaji kukimbilia usalama wao.
Walisema kuwa Igiebor hakubahatika kwani jiwe
liligonga mkono wake na kusababisha damu kuvuja sana
Super Eagles wa Nigeria ndio wanaonekana kuwa katika
nafasi nzuri ya kufuzu kucheza katika michuano ya kuwania kombe la dunia
watakapocheza mechi ya marudiano mjini Calabar tarehe 16 Novemba.
0 comments