Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
akikabidhi jezi kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA),
Amos Kafyunga, pembeni kushoto ni nahodha wa timu ya Taifa ya Pool, Chaerles
Venance na kulia ni Meneja wa timu hiyo, Nabil Hizza.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya
Safari Lager imetoa Sh 67 milioni kuidhamini timu ya Taifa ya Tanzania ya
mchezo wa Pool katika ushiriki wake wa mashindano ya Afrika ya mchezo huo
yatakayofanyika nchini Malawi.
Akizungumza na Nyumba ya Michezo na Burudani leo,
Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema fedha hizo walizotoa
zitatumika katika kulipia gharama za usafiri, malazi na posho kwa kipindi chote
timu itakapokuwa safarini.
Shelukindo alisema nia ya TBL kupitia Safari Lager
kudhamini timu hiyo ni kuendleza mchezo wa Pool sambamba na kuibua vipaji vya
vijana na kuwasaidia kiuchumi.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), pembeni yake kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA),
Amos Kafyunga, kushoto ni nahodha wa timu ya Taifa ya Pool, Chaerles
Venance na kulia mwisho ni Meneja wa timu hiyo, Nabil Hizza.
Kwa upande wake, Meneja wa timu hiyo, Nabil Hizza
aliwataja wachezaji ambao wameingia kambini katika hoteli ya Picolo iliyopo
Kawe, kuwa ni Mohamed Idd, Festo Yohana, Patrick Nyangusi, Omari Akida, Fred
Steven, Geofrey Swai, Abdallah Hussein, Innocent Sami na nahodha wao Charles
Venance.
Timu hiyo kabla ya kwenda kwenye mashindano hayo
yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu, inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na
timu ya taifa ya Kenya mchezo utakaochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Arusha.
0 comments