PAMOJA na nahodha wa timu ya Taifa ya Cameroon,
Samuel Eto’o kurudi katika kikosi chake lakini jana usiku alishindwa kuisaidia
timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya Tunisia katika mchezo wa kuwania kufuzu
kucheza Kombe la Dunia la Brazil 2014.
Eto’o ambaye alistaafu kuichezea timu hiyo lakini
alirudi baada ya kuombwa na rais wa nchi hiyo, lakini pamoja na kuwa uwanjani
timu yake ilimaliza mchezo huo uliochezwa jijini Tunis kwa suluhu.
Miamba hiyo inatarajia kurudiana tena Novemba 17
jijini Yaunde na matokeo ya mchezo huo ndiyo yatatoa nani anaweza kutinga
nchini Brazil kushiriki fainali hizo kati yao.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani katika
dakika zote 90, Tunisia walikuwa wakiliandama lango la wapinzani wao lakini shukrani
kwa kipa wa zamani wa Liverpool, Charles Itandje ambaye aliisaidia Camerron
kuokoa michomo mingi langoni kwake.
Timu hizo zote zimeshacheza kombe la dunia mara tisa
hivyo wanawania nafasi ya 10 kucheza michuano hiyo mikubwa duniani, hivyo
ushindani katika mchezo wa marudiano utakuwa mkubwa zaidi ya jana usiku.
0 comments