Open top menu
Jumapili, 6 Oktoba 2013


Beki wa Mtibwa Sugar, Paul Ngalema akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza.

MABAO mawili ya Mrisho Ngassa na Didier Kavumbagu yameiwezesha Yanga kuikaribia Simba wanaoongoza Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kufikia pointi 12 nyuma pointi tatu na vinara hao.

Yanga ambao walianza ligi hiyo kwa kususua wamefanikiwa kuibakiribia Simba baada ya kuibua na ushindi huo dhidi ya Mtibwa Sugara katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga ambao leo walikuwa uwanjani bila kiungo wao Haruna Niyonzima ambaye anasumbuliwa na matatizo ya kifamilia, walianza kupata bao la kwanza dakika ya sita kupitia kwa Ngassa kabla ya Kavumbagu kutupia bao la pili dakika ya 24.

Katika mchezo mwingine uliochezwa jijini Tanga, Mgambo walishindfwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Prisons mfungaji akiwa Peter Michael dakika ya 72.
 Mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza akilimiki mpira mbele ya beki wa Mtibwa, Hassan Ramadhani
 Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu akiwajibika.
 Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu akifunga bao la pili katika mchezo huo, huku kipa wa Mtibwa, Hussein Ashiraf akigaagaa
 Mrisho Ngassa akishangilia baada ya kufunga bao lake la kwanza toka alipojiunga na Yanga kwa mara ya pili.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments