Open top menu
Jumanne, 8 Oktoba 2013


UWANJA wa klabu ya AC Milan wa San Siro umefungwa kwa mashabiki kuingia uwanjani kushuhudia mechi ijayo ikiwa ni sehemu ya adhabu iliyotolewa na Chama cha Soka Italia baada ya mashabiki wa timu hiyo kuporomosha matusi katika mchezo wao wa juzi.

Hii ni mara ya pili kwa Milan kukumbwa na hatua kama hii iliyoidhinishwa na Jaji wa Ligi ya Serie A.

Hukumu hio itaanza kwenye mechi ijayo dhidi ya Udinese iliyopangwa tareh 19 Oktoba. Pamoja na marufuku hio klabu imetozwa faini ya takriban dola za Marekani 68,000.

Kwingine Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michezl Platini amesema kua mchezo huo unafaa kuongoza juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi katika michezo.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments