DEREVA wa timu ya mbio za magari yaendayo kasi ya
Formula One ‘Langalanga’ wa Redbull, Sebastiani Vettel amewadhihirishia mapenzi
wa mashindano hayo kuwa hana mpinzani kwa sasa baada ya kutawazwa kuwa bingwa
wa mbio hizo mwaka huu huku kukiwa bado mashindano hayo yajamalizika.
Vettel ametangazwa kuwa bingwa wa Langalanga 2013
jana usiku baada ya kushinda mbio zilizofanyika nchini India huku kukiwa badoi
kumebakia na mashindano matatu ya mbio hizo.
Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 26 aliendesha
gari lake bila matatizo yoyote kufanikisha ushindi wake wa mara ya sita
mfululizo msimu huu na kujitokeza kuwa dereva wa nne katika historia ya
mashindano haya kufanya hivyo.
Baada ya mbio hizo Vettel alisema, nashindwa hata
kusimulia, nimevuka msitari wa kumaliza mbio nikapoteza kauli. Najitahidi
kutafuta maneno lakini nashindwa. Ni msimu mzuri kwake, timu yake ina furaha kubwa sana.
Ushindi huu ni wa sita mfululizo na wa kumi kwa
ujumla wa msimu mzuri kwake ambao unaweza kumsogeza karibu na rekodi
inayoshikiliwa na Schumacher aliyeshinda jumla ya mbio 13 katika msimu mmoja.
Licha ya uwezo wake wa kushinda hata hivyo, Vettel
ameshindwa kuwa na mvuto katika ushindi wake. Mfano ni ushindi wake huko
Ubelgigi, Uingereza, Canada na Singapore ambako alizomewa na kwenye medani ya
India alisimulia na jinsi kuzomewa huko kulivyomuathiri.
Amesema kuwa nilizomewa ingawa sikufanya kosa lolote
na hilo liliniudhi kiasi lakini majibu nimeyatoa kwa ushindi uwanjani.
Endapo Vettel atashinda mbio tatu zilizosalia huko
Abu Dhabi, Marekani na Brazil atafikia pia ushindi wa mara tisa wa Albert
ASCARI wa mwaka 1952 na 1953.
Hata hivyo mpango mpya wa utaratibu utakaoanza mwaka
2014 kuendelea mbele ukihusisha mfumo mpya wa Ingini za magari pamoja na mfumo
wa kuwezesha ingini ziongezewe nguvu --yanaweza kuzidisha ushindani wa mbio
hizi.
0 comments