Open top menu
Jumatatu, 7 Oktoba 2013


BINGWA wa zamani wa dunia wa uzito wa kati, Karama Nyilawila amemvaa bondia wa uzito wa huo kwa sasa, Thomas Mashali wa Tanzania kuwa yupo tayari kupambana naye wakati wowote.

Mashali ambaye alitwaa ubingwa huo hivi karibuni kutoka kwa Mtanzania mwenzake, Mada Maugo katika mpambano uliofanyika nchinio miezi kadhaa iliyopita.

Nyalawila aliiambia Nyumba ya Michezo na Burudani, kuwa yupo fiti kuurudisha ubingwa wake kutoka kwa Mashali kwani anaamini bondia huyo hana uwezo wa kumpiga wakati wowte atakaopambana naye.

Bondia huyo alisema kuwa Mashali aliupata mkanda huo kwa bahati na akikubali kupanda ulingoni kupigana naye ndiyo utakuwa mwisho wa kuitwa bingwa wa dunia wa uzito huo.

“Namtaka Mashali wakati wowote ule, niliwahi kupigana naye nikiwa naumwa marelia lakini tulitoka sare tena kwa maamuzi yenye utata,” alisema Nyalawila.

Nyilawila Oktoba 20 mwaka huu anatarajia kupanda ulingoni kupambana na Sado Philemon mpambano uliopangwa kufanyika kwenye Ukumbi wa CCM Mwinjuma.

Karama Nyilawila akiruka juu baada ya kutangazwa mshindi wa ubingwa wa dunia wa uzito wa kati alipotwaa ubingwa huo huko Ulaya.

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments