Wachezaji wa West Ham United wakishangilia moja ya mabao yao katika mchezo wao dhdi ya Tottenham Hortspur jana usiku.
LIGI Kuu ya England jana iliendelea katika viwanja
tofauti lakini michezo iliyokuwa gumzo ni kati ya West Ham United na Tottenham
Hortspur, Arsenal dhidi ya West Brom huku Chelsea ikiwavaa Norwich City.
Katika michezo hiyo timu ya Tottenham walijikuta
wakiangukia pua wakiwa nyumbani baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka
kwa West Ham United mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa White Hart Lane
Arsenal nao waliponea kwenye tundu la sindano
kupoteza mchezo wao ambao walikuwa ugenini baada ya kutoka sare ya mabao 1-1
dhidi ya West Brom ambao walitangulia kupata bao na Arsenal kuchomoa kipindi
cha pili.
Lakini kwa upande wa Chelsea wao walifanikiwa kuvuna
pointi tatu baada ya kuinyuka Norwich mabao 3-1 katika mcheoz huo ambao ulikuwa
na ushindani mkubwa.
Hakuna mtu aliyetarajia kwamba Tottenham wangechapwa
namna hivyo hasa kwa kuzingatia kuwa ndiyo iliyovunja rekodi ya pesa nyingi za
kuwanunua wachezaji wapya.
Mabao ya West Ham katika mchezo huo yalifungwa na Winston
Reid dakika ya 66 na Ricardo Vaz Te akafunga bao la pili dakia sita baadae na Ravel
Morrison ndiye aliyefunga bao la tatu.
Huo ni ushindi wa kwanza wa West Ham kwenye uwanja
wa White Hart Lane tangu mwaka 1999 na ni ushindi wa kwanza wa ugenini tangu
msimu huu kuanza. Katika mchezo mwingine Southamptom waibugiza Swansea 2-0.
0 comments