Open top menu
Ijumaa, 4 Oktoba 2013


 MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Buibui amefyatua single yake mpya alioipa jina la Hii Ngoma ikiwa pamoja na style yake mpya ya kucheza ya Kichichi mawe.

Buibui aliiambia Nyumba ya Michezo na Burudani kuwa baada ya kimya cha muda mrefu sasa amerudi rasmi katika tasnia ya muziki na wimbo wa Hii Ngoma ni ujio wake mpya.

Akizungumzia style yake ya Kichichi mawe, Buibui alisema ameamua kutumia style hiyo ambayo ameitoa katika jina la bondia Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ ikiwa ni sehemu ya kumpongeza mwanamasumbwi huyo kwa kufanya vizuri kwa sasa.
Buibui akiwa na bondia Francis Miyeyusho 'Chichi Mawe'

Kichichi mawe ni aina ya mchezo mpya wa kucheza na  ni njia pia ya kupongezana, Miyeyusho kwani ni rafiki yangu wa karibu sana. Kila nitakapokuwa jukwaani au kwenye video zangu nitakuwa natumia mtindo huo wa kucheza,” alisema Buibui alipokuwa anaongea na Nyumba ya Michezo na Burudani.

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments