MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) iliyochezwa jana
(Oktoba 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Yanga na Mtibwa
Sugar imeingiza sh. 97,557,000.
Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo
namba 46 lililochezeshwa na Isihaka Shirikisho kutoka Tanga walikuwa 17,313.
Yanga ilishinda mabao 2-0.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh.
8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh.
23,453,748.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
14,881,576.27.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya
uwanja sh. 11,925,635.06, gharama ya kuchapa tiketi ni sh. 3,171,190 wakati
gharama za mchezo ni sh. 7,155,381.04.
Kamati ya Ligi sh. 7,155,381.04, Mfuko wa Maendeleo
ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,577,690.52 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,782,648.18.
0 comments