TIMU ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 20 (Serengeti Boys) imealikwa kushiriki Olimpiki ya Afrika
itakayofanyika Mei mwakani.
Mpira wa miguu ni kati ya michezo 22
itakayoshindaniwa katika mashindano yatakayofanyika Gaborone, Botswana chini ya
Kamati za Olimpiki za Afrika (ANOCA).
Kwa mujibu wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC),
Tanzania imepewa nafasi ya kushiriki katika michezo hiyo ya Olimpiki kwa Afrika
kutokana na kuwa na programu nzuri za vijana hasa chini ya umri wa miaka 17.
Hiyo itakuwa ni michezo ya Pili ya Afrika kwa
Olimpiki ambapo ya Kwanza ilifanyika mwaka 2010 jijini Rabat, Morocco.
0 comments