Tenga akimkabidhi mpira Malinzi kuashiria yeye ndiye kiongozi mpya mkuu wa soka nchini
JAMAL Emil Malinzi, usiku huu ameshinda Urais wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupata kura 72, dhidi ya 52 za
mpinzani wake Athumani Jumanne Nyamlani.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa
NSSF Water Front, Dar es Salaam, Walace Karia alifanikiwa kushinda nafasi ya
Makamu wa Rais kwa kupata kura 67 akiwashinda Nassib Ramadhani kura 52 na Imani
Madega sita.
Huyu ndiye Rais wenu mpya TFF; Rais aliyemaliza muda
wake TFF, Leodegar Tenga kushoto akimtambulisha Jamal Malinzi kulia kuwa Rais
mpya wa shirikisho.
Katika nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13; kiungo wa
zamani wa Simba SC Wilfred Kidau amepata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said kura
50, Omar Abdulkadir kura 10 na Alex Kabuzelia kura nne.
Kanda 12; Khalid Mohamed Abdallah amepata kura 69 na
kumshinda Davisa Mosha aliyepata kura 54.
Kanda ya 11 Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amepata kura 78
na kuwashinda Riziki Majala kura tano, Twahir Njoki kura mbili, Juma Pinto kura
26 na Farid Mbaraka kura 14, Kanda ya 10 ameshinda Hussein Mwamba aliyepata
kura 63, huku Charles Komba akipata nne na Stewart Nasima 58.
Kanda ya tisa Othman Kambi aliyepata kura 84 yeye
amewashinda Francis Bulame kura 30, wakati James
Anampa shada la maua ishara ya kumuachia madaraka
Kwaherini; Tenga akiwaaga Wajumbe
Mhagama aliyepata 93 amemshinda Zafarani Damoda
aliyepata kura 11 na Kanda ya nane, Ngube Kiondo amepata kura 73 amemshinda
Ayoub Nyaulingo kura 52.
Kanda ya Tano, Ahmed Iddi Mgoyi aliyepata kura 92
amemshinda Yussuf Kitumbo aliyepata kura 34, wakati Kanda Omar Walii Ali
amepata kura 53 dhidi ya 19 za Ally Mtumwa.
Anamkabidhi Katiba ya TFF
Eley Mbise amepata kura 51 dhidi ya 53 kura 57 za Lamanda Swai.
Mbasha Matutu aliyepata kura 63, amembwaga Vesastis
Ligano aliyepata kura 61, wakati Vedastus Lufano aliyepata kura 51, amewashinda
Jumbe Odesa Magati kura 11, Mugisha Galibona kura 24 na Samuel Nyalla kura 39
na Kanda namba moja, Karilo Samson hakuwa na mpizani akapita moja kwa moja.
Kamati mpya ya Utendaji ya TFF
Habari na Picha kwa Hisani ya Bin Zubeiry
0 comments