Open top menu
Jumatano, 16 Oktoba 2013


Wachezaji wa England walkishangilia bao la pili lililofungwa na Gerrard na kuwahakikishia kucheza fainali za Kombe la Dunia Brazil.

MABAO mawili yaliyofungwa na mshambuliaji England, Wayne Rooney na kiungo wao, Steven Gerrard yalitosha kuipeleka Three Lions kukata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 Brazil.

England walikuwa wanahitaji ushindi pekee katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Wembley jijini London, walicheza kufa au kupona kuhakikisha wanashinda mchezo huo.

Huku wakiwa wanashangilia na mashabiki wao kwenye uwanja wa nyumbani, England walianza kupata bao la kwanza dakika ya 41 kupitia kwa Rooney kabla ya Gerrard kukwamisha bao la pili dakika ya 88 ya mchezo huo.


Kiungo wa England, Steven Gerrard akifunga bao la pili akiwa katikati ya wachezaji wa Poland na kuihakikishia timu yake kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014 zitakazofanyika nchini Brazil.
Mshambuliaji wa England, Daniel Sturridge akiwatoka wachezaji wa Poland.

Wayne Rooney akimtoka beki wa Poland, Grzegorz Krychowiak katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Mshambuliaji wa England, Wayne Rooney akifunga bao la kwanza katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil dhidi ya Poland uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Wembley.


MATOKEO YA MICHEZO MINGINE YA KUWANIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA BARANI ULAYA HAYA HAPA
Ubelgiji     1 - 1  Wales
England     2 - 0  Poland
Ufaransa    3 - 0  Finland
Montenegro        2 - 5  Moldova
San Marino         0 - 8  Ukraine
Scotland    2 - 0  Croatia
Hispania    2 - 0  Georgia
Faroe          0 - 3  Austria
Jamhuri Ireland  3 - 1  Kazakhstan
Italia         2 - 2   Armenia
Sweden      3 - 5  Ujerumani
Serbia        5 - 1  Macedonia
Bulgaria     0 - 1  Czech
Denmark    6 - 0  Malta
Latvia         2 - 2  Slovakia
Hungary    2 - 0  Andorra
Norway      1 - 1  Iceland
Romania    2 - 0  Estonia
Switzerland         1 - 0  Slovenia
Uturuki      0 - 2  Uholanzi
Azerbaijan 1 - 1  Russia
Ugiriki       2 - 0  Liechtenstein
Israel 1 - 1  Ireland
Lithuania   0 - 1  Bosnia
Ureno         3 - 0  Luxembourg
Cyprus       0 - 0  Albania
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments