Open top menu
Jumamosi, 12 Oktoba 2013


KLABU ya Simba leo imeendelea kung’ang’ania kileleni baada ya kuitandika Tanzania Prisons bapo 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wakati Simba ikikaa kileleni baada ya kujikusanyia pointi 18,  watani wao Yanga nao wamezidi kuwakalia kooni baada ya kuinyuma Kagera Sugar wakiwa uwanja wa nyumbani mabao 2-1.

Yanga baada ushindi huo wamerudi katika nafasi yao ya pili baada ya kufikisha pointi 15  hivyo mchezo wa watani hapo wa jadi wa Oktoba 20 ndiyo utakaoamua nani atakaa kileleni au kumfikia mwenzake.

Bao pekee la Simba lilifungwa na Jonas Mkude kwa shuti la mbali nje ya eneo la hatari na kumshinda mlinda mlango wa Prisons Beno David na mpira kukwama wavuni.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza wakati bao la Kagera lilikwamishwa wavuni na Godfrey Wambura.

Mchezo mwingine wa Ligi hiyo uliochezwa kwenye Uwanja wa Chamanzi Ashanti United walizinduka na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union.



  
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments