NAHODHA wa zamani wa England, Rio Ferdinand na Kocha
wa timu hiyo, Roy Hodgson ameongezwa katika Tume iliyoundwa na Chama cha Soka
cha England (FA) kwa lengo la kuboresha kikosi cha timu ya Taifa ya England,
Three Lions kitakachoshiriki fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Ferdinand na Hodgson wameongezwa ikiwa siku moja
baada ya Heather Rabbatts kuikosoa FA kwa kuchagua wajumbe wazungu pekee kuunda
tume hiyo ambayo itakuwa na kazi ya kutoa mapendekezo ya kuiboresha gtimu hiyo
kabla ya kushiriki fainali hizo.
Hodgson, 66, ndiye aliyeiwezesha timu ya England kutinga
katika fainali hizo za 2014 zitakazofanyika nchini Brazil mwakani wakati Ferdinand,
34, aliichezea timu hiyo michezo 81 kabla ya kuamua kustaafu mwezi Mei mwaka
huu.
Mwenyekiti wa FA, Greg Dyke alisema Ferdinand alikuwa
katika mipango ya kujumuishwa katika tume hiyo kwani ana umuhimu mkubwa.
"Tumezungumza na Rio na klabu yake ya Manchester
United kwa vipindi tofauti juu ya kumjumuisha katika tume hiyo kabla ya kutaja
jina lake," alisema Dyke.
"Kwa sasa Ferdinand anaitumikia klabu ya Manchester
United tulikuwa tunahitaji kupata uhakika kama ataweza kuhudhuria katika kamati
hiuyo pindi atakapohitajika. Tumekubaliana kuwa ataweza kuifanya kazi hii
tuliyompa."
Ferdinand na Hodgson wataungana na Makamo Mwenyekiti
wa FA, Roger Burden, Kocha wa zamani wa England, Glenn Hoddle, beki wa zamani
wa England, Danny Mills, Meneja wa Mwenyekiti wa FA, Howard Wilkinson, Ritchie
Humphreys, Mweniekiti wa ligi, Greg Clarke mna Dario Gradi.
0 comments