Kiungo wa England, Jack Wilshere
KAULI iliyotolewa na kiungo wa Arsenal na timu ya
taifa ya England, Jack Wilshere ni sawa na kumtimua kinda wa Manchester United,
Adnan Januzaj ambaye amekuwa akipigiwa debe kuichezea England.
Wilshere alipoulizwa juu ya sakala hilo alijibu, ‘Waingereza
pekee ndiyo wanatakiwa kuichezea timu ya taifa ya England’.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, alimesajiliwa na
Manchester United msimu huu anaweza kuichezea England kama akipata kibari
kutoka Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) baada ya kuishi nchini humo kwa miaka
mitano.
Kiungo huyo ambaye wiki iliyoipita aliisaidia timu
yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sunderland kwa kufunga mabao yote
mawili ana uhuru wa kuchagua timu moja ya taifa ya kuichezea kati ya Ubelgiji, Serbia,
Albania na Uturuki.
Kinda la Manchester United, Adnan Januzaj akishangilia moja ya mabao yake akiwa na wachezaji wenzake
Wilshere alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema:
"Kama umeishi England kwa miaka mitano haimaanishi kuwa wewe ni Mwingereza."
“Tuna wachezaji wengi sana katika kikosi cha timu
yetu ambao hawajazaliwa hapa na familia zao pia hazipo hapa nchini lakini
hawazichezei hizo nchi walikokuwa wazazi wao.”
0 comments