Open top menu
Jumanne, 8 Oktoba 2013


KOCHA Gus Poyet ametangazwa kuwa Kocha mkuu wa timu ya Sunderland, kuchukua mikoba ya Paolo Di Canio aliyetimuliwa hivi karibuni kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Sunderland The Black Cats, ambao wanaburuza mkia kwenye Ligi Kuu ya England, walimtimua kazi Di Canio baada ya kuiongoza timu hiyo kwa michezo 13 ya msimu uliopita na msimu huu.

Poyet, 45, amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake Stadium of Light.

Mwenyekiti wa Sunderland, Ellis Short amesema wametazama kocha kwa mapana yake na kugundua miongoni mwa orodha yao Poyet ana rekodi nzuri, uzoefu, mwenye kuwajibika, mapenzi ya kazi na hivyo wameona ndiye mtu sahihi.

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments