TIMU ya Taifa ya Zambia Chipolopolo ikiwa chini ya
kocha wa mpito Patrice Beaumelle inashuka dimbani leo kukipiga dhidi ya
mabingwa wa dunia mara tano Brazil kwenye mchezo wa kirafiki utakaopigwa kwenye
Uwanja wa Birds Nest.
Mabingwa hao wa zamani wa Africa watakuwa bila ya
mshambuliaji Rodger Kola, Collins Mbesuma, kiungo Mukuka Mulenga na beki Davies
Nkausu ambao ni majeruhi.
Pia wachezaji Nathan Sinkala, Stopilla Sunzu,
Rainford Kalaba wameshindwa kuripoti kwa wakati kwenye maandalizi ya mchezo
huo.
Lakini kocha Beaumelle anaamini atachezesha kikosi
imara na inawezekana akaamua kuwaanzisha wachezaji wanaocheza ligi ya nyumbani
Bronson Chama, Kondwani Mtonga na Bruce Musakanya ambao watachanganywa na
wazoefu Hichani Himonde, Kampamba Chintu na Joseph Musonda lakini pia
inawezekana wakacheza Jimmy Chisenga au Emmanuel Mbola.
Nahodha Christopher Katongo, Noah Chivuta, Chisamba
Lungu na Fwayo Tembo wapo kamili kuitumikia Zambia kwenye mchezo huo ambapo
Jacob Mulenga kuongoza mashambulizi na James Chamanga huku Emmanuel Mayuka
likiwa ni chaguo lingine.
Brazil kwa upande wao watakuwa bila ya kipa Julio
Cesar, beki Thiago Silva na mshambuliaji Fred.
Felipe Luiz Scolari anatarajia kufanya mabadiliko
kadhaa Diego Cavalieri atambadili Jefferson langoni wakati Daniel Alves, Dedé,
David Luiz na Maxwell watatengeneza ukuta.
Lucas Leiva, Paulinho na Ramires wanatarajiwa kuanza
kwenye kiungo huku Lucas, Alexandre Pato na Jo wakiwa kwenye ushambuliaji.
Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana
0 comments